chat

NGUZO ZA SWALA

NGUZO ZA SWALA

NGUZO ZA SWALA

shiriki:



Nguzo Za Swalah, Vitendo Vya Waajib Na Sunnah Katika

Swalah

imekusanywa na Abubakari shabani Rukonkwa.

imerejewa na Ummu Rahma

Swalah

Nguzo za Swalah ni 14: Nguzo ni zile ambazo ukiswali na

ukaziacha kwa makusudi Swalah yako inabatilika, na ikiwa

umeacha kwa kusahau, Swalah yako pia itakuwa haikukamilika

hadi urejee kitendo chenyewe au urejee rakaa na kisha

mwishoni utoe Sajdatus-Sahw. Lakini ukiwa umesahau nguzo

ya Takbiyratul-Ihraam, basi itakubidi uiswali Swalah upya tokea

mwanzo.

Nguzo hizo 14 ni hizi zifuatazo:

1. Kusimama katika Swalah za Fardh kwa yule mwenye uwezo.

(Wanachuoni wengine wamesema nguzo ya kwanza ni Niyah

kabla ya Kusimama). Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:

"Na simameni kwa ajili ya Allaah hali ya kuwa watiifu" (Al-

Baqarah: 238).

Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

amesema: "Swali hali ya kuwa umesimama, usipoweza, basi

kwa kukaa na usipoweza basi kwa kulala ubavu" (Al-Bukhaariy

na Abu Daawuud).

2. Takbira ya kuhirimia (Takbiyratul-Ihraam) kwa tamko la


Allaahu Akbar kutokana na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu

'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ufunguo wa Swalah ni

kujitwaharisha, na kuifunga ni Takbira, na kuifungua ni kutoa

Salaam" (Abu Daawuud na At-Tirmidhiy).

3. Kusoma Suratul-Faatihah katika kila rakaa. Mtume (Swalla

Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema: "Hapana Swalah

kwa ambaye hakusoma Suratul Faatihah" (Al-Bukhaariy).

4. Kurukuu.

5. Utulivu (Twumaaniynah) katika Rukuu.

6. I'itidaal (hapa inaingia na kunyanyuka kutoka katika Rukuu

hadi anaponyooka mtu).

7. Utulivu katika I'Itidaal.

8. Kusujudu.

9. Utulivu katika kusujudu. Kutulia wakati wa kurukuu,

kusujudu, kusimama, kukaa baina ya Sijdah mbili kwa msemo

wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Kisha

rukuu mpaka utulizane hali ya kurukuu, kisha nyanyuka mpaka

ulingane sawa hali ya kusimama, kisha sujudu mpaka utulizane

na hali umesujudu, kisha nyanyuka mpaka utulizane hali ya

kuwa umekaa" (Al-Bukhaariy).

10. Kikao baina ya Sijda mbili.

11. Utulivu katika kikao baina ya Sijda mbili.

12. Tashahhud ya mwisho.

13. Kikao katika Tashahhud ya mwisho.

14. Salaam (Kutoa Salaam) ya kwanza.

Utahakikisha unafuatanisha yote hayo kama utaratibu

ulivyopangika.

Waajib Za Swalah(VIPASAJI)

Ni lile ambalo ni wajibu kulifanya au kusema, inaondoka kwa

kusahau na kulazimisha mwenye kuswali kusujudu sijdah mbili

za kusahau. Yeyote mwenye kuacha kwa kusudi Swalah yake

inabatilika ikiwa anajua uwajibu wake.

Istilahi hii inatumika kwa madhehebu ya Hanafi na Hanbali ila

ma-Hanafi hawaoni kuwa mwenye kuacha wajibu kwa kusudi

inabatilisha Swala yake bali yeye amefanya madhambi

anayostahiki adhabu. Ama ma-Maaliki na ma-Shaafi'y hawana

kigawanyo hichi cha Waajib kwao ila wao wana nguzo na

Sunnah kwa ujumla wake.

Ama hapa tutaweka yale yaliyotajwa ambayo yanaelekea kuwa

na nguvu zaidi.

Kwanza kabla hatujataja mambo yenyewe, tunapaswa kujua

kuwa mambo ya Waajib ni yale ambayo vilevile atakapoacha

mtu kwa makusudi hubatilika Swalah yake, na atakapoacha kwa

kusahau inamtosheleza yeye kusujudu Sijda mbili za kusahau

'Sujuudus-Sahw'.

Ama mambo ya Waajib ambayo yametajwa katika kitabu cha

'Swahiyhu Fiqhus-Sunnah' kwa dalili mbalimbali za Aayah na

Hadiyth ni 9 kama yafuatayo:

Du'aa ya ufunguzi wa Swalah 'Du'aa al-Istiftaah'.

Kusema 'A'udhu biLlaahi Minash-Shaytwaan ar-Rajiym' kabla

ya kusoma 'BismiLlaah ar-Ramaanir Rahiym' na 'Suratul-



Faatihah'.

Kusema 'Aamiyn' baada ya Suratul-Faatihah.

Takbiyrah za kuhama baina ya kitendo na kitendo.

Kusema 'Sami'aLlaahu liman hamidah'Kusema 'Rabbana Lakal

Hamdu' katika I'itidaal.Kusema 'Subhaana Rabbiyal 'Adhwiym'

wakati wa kurukuu na kusema 'Subhaana Rabbiyal A'ala' wakati

wa kusujudu.Tashahhud ya kwanza.Kikao cha Tashahhud ya

kwanza.

Wanachuoni wengine wametaja mambo ya Waajib ni 8 kama

yafuatayo:

Takbiyrah nyingine zote isiyo ile ya Ihraam.Kusema

'Sami'aLlaahu liman hamidah' kwa Imaam na mwenye kuswali

peke.

Kusema 'Rabbana Lakal Hamdu'.Kusema 'Subhaana Rabbiyal

'Adhwiym’ mara moja kwenye kurukuu.

Kusema 'Subhaana Rabbiyal A'ala' kwenye kusujudu.

Kusema 'Rabbi-Ghfir liy' kwenye kikao baina ta Sijda mbili.

Tashahhud ya mwanzo.Kikao katika Tashahhud ya

mwanzo.Hizi ndizo maarufu zaidi kwa wanachuoni wengine.

Sunnah Za Swalah

Hizi ni kauli na vitendo zinazopendeza kuletwa katika Swalah.

Mwenye kufanya hayo hupata thawabu wala Swalah haibatiliki

kwa kuachwa hata kwa kusudi. Wala sijdah ya kusahau hailetwi.

Hapa tuna vigawanyo viwili vya Sunnah katika Swalah; Sunnah

za kauli na Sunnah za vitendo.

Sunnah Za Kauli

Kisomo baada ya al-Faatihah.Dhikr nyinginezo katika Rukuu.

Dhikr baada ya kusimama kutoka katika Rukuu na baada ya

kusema ‘Rabbana Lakal Hamd’.Dhikr nyinginezo katika

Sujuud.Du’aa baina ya Sijdah mbili.Kumswalia Mtume (Swalla

Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika Tashahhud ya

kwanza na ya pili.Du’aa baada ya Tashahhud ya kwanza na ya

pili.Salaam ya pili.

Dhikr na du’aa mbalimbali baada ya Swalah.

Sunnah Za Vitendo

Kuweka Sutrah (kizuizi mbele ya sehemu unayoswalia) katika

Swalah.

Kunyanyua mikono wakati wa Takbiyratul Ihraam, na wakati

wa kurukuu na na wakayi wa kunyanyuka kwayo na wakati wa

kuinuka kutoka katika Tashahhud ya kwanza. Na kadhalika

wakati unapoinama na kuinuka.Kuweka mkono wa kuume juu

ya mkono wa kushoto juu ya kifua unaposimama kuswali.

Kutazama mahali pa kusujudu.

Kulingana sawa mgongo unaporukuu na kutonyanyua kichwa au

kukiinamisha sana, na kuweka viganja kwenye magoti mawili

na huku umeviachanisha vidole vya mikono na kuachanisha

viwiko visiguse mbavu au tumbo lako.

Kuteremka katika Sijdah kwa mikono miwili kabla ya magoti

(Wengine huona kushuka kwa magoti kabla ya mikono).

Kuimakinisha paji la uso, pua na mikono (viganja viwili)

kwenye ardhi pamoja na kupanua mikono isiguse mbavu zako;

kuwe na uwazi wa kuweza kupita kinyama kidogo. Na viganja

vyako viwe usawa wa mabega au masikio wakati uko katika

kusujudu na viwiko vikiwa vimenyanyuliwa juu na vidole vya

mikono vikiwa vinaelekea Qiblah. Matumbo ya vidole vya

miguu yakiwa ardhini visigino vikielekea juu na hali vidole vya

miguu vikielekea Qiblah.Kulilalisha guu la kushoto na

kulisimamisha la kulia wakati wa kikao baina Sijdah mbili.

Kurefusha kikao baina ya Sijdah mbili.Kikao cha mapumziko

baada ya kukamilisha rakaa ya kwanza na ya tatu.Kutegemea

ardhi kwa mikono wakati mtu anaponyanyuka kutoka kusujudu

na kwenda kwenye rakaa nyingine.

Kukaa kikao cha Iftiraash (Kusimamisha mguu wa kulia na

kukalia mguu wa kushoto) katika Tashahhud ya mwanzo. Na

kukaa kikao cha Tawarruk (kusimamisha mguu wa kulia na

kuipitisha mguu wa kushoto chini ya muundi wa mguu wa kulia

na huku kikalio chako kimekaa juu ya ardhi).

Kuashiria kwa kidole cha shahada katika Tashahhud kuanzia

mwanzo hadi mwisho bila kukishusha na huku unasoma na

ukikitazama.

(Abu Maalik Kamaal Saalim, Swahiyh Fiqhus Sunnah, Mj. 1).

Hata hivyo, Shaykh Abu Bakar Jaabir al-Jazaairiy katika kitabu

chake Minhaajul Muslim yeye amegawanya Sunnah za Swalah

katika mafungu mawili: Zilizotiliwa mkazo kama vile Waajib na

zisizotiliwa mkazo.

Sunnah Zilizotiliwa Mkazo

Kusoma Surah au Aayah katika Qur-aan baada ya Suratul

Faatihah katika Swalah ya Asubuhi, rakaa mbili za mwanzo za

Swalah ya Adhuhuri, Alasiri, Maghrib na 'Ishaa.

Kusema ‘Sami'a Alaahu liman Hamidah’ wakati wa kuitadili na

kisha Rabbaana walakal Hamd, Subhaana Rabiyal 'Adhiym

wakati wa kurukuu, Subhaana Rabiyal A'alaa wakati wa

kusujudu.

Takbira ya kuhama.

Tashahhud ya kwanza na tamko lake.Kusoma kwa uwazi katika

Swalah ya kusoma kwa uwazi na kusoma kwa siri katika Swalah

ya kusoma kwa siri.Kumswalia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi

wa aalihi wa sallam) katika Tashahhud ya mwisho.

Sunnah Zisizotiliwa Mkazo

1. Du'aa ya ufunguzi.

2. Kusoma A’udhubiLlaah.

3. Kunyanyua mikono miwili mpaka usawa wa mabega.

4. Kusema Aamiyn.

5. Kurefusha kisomo katika Swalah ya Asubuhi na kupunguza

katika Swalah ya Alasiri na Maghribi.

6. Namna ya mkao, nayo ni kukalia mguu katika vikao vyote na

kukalia tako katika kikao cha mwisho. Mikao ni wa Iftiraash


(kukalia tumbo la mguu wa kushoto na kuunyoosha unyayo wa

mguu wa kulia) na Tawarruk (kuweka tumbo la mguu wa

kushoto chini ya paja la kulia na kuweka kikalio ardhini na

kunyoosha unyayo wa mguu wa kulia).

7. Kuweka mikono juu ya kifua, wa kulia juu ya wa kushoto.

8. Du'aa katika Sijdah.

9. Du'aa katika Tahiyyaatu.

10. Kuanzia kulia kutoa salaam.

11. Kutoa salaam ya upande wa kushoto.

Ingawa kuna ikhtiliaaf ya hao wanachuoni, tunapenda

kuwakumbushia Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa

aalihi wa sallam)aliyesema: "Swalini kama mlivyoniona

nikiswali" (Al-Bukhaariy).

Kwa hivyo, ni juu yetu kufanya juhudi kufuata yote aliyofanya

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ili tuchume

thawabu nyingi zaidi.

Allah ndie mjuzi zaidi.